Skip to content

Opening book details…

Can I read Maisha yangu: Miaka minane ndani ya baraza la mapinduzi: Khaini au mhanga wa mapinduzi ? on EtoBox?

Maisha yangu: Miaka minane ndani ya baraza la mapinduzi: Khaini au mhanga wa mapinduzi ? by Khamis Abdulla Ameir is a nonfiction available to read on EtoBox.

What is Maisha yangu: Miaka minane ndani ya baraza la mapinduzi: Khaini au mhanga wa mapinduzi ? about?

Khamis Abdulla Ameir anasimulia hadithi ya maisha yake kwa ari na shauku kubwa - hadithi ambayo siyo ya kubuni bali ni ya kweli kabisa juu ya mambo yaliyotokea Zanzibar katika kipindi cha kilele cha Vita Baridi, COLD WAR, baina ya nchi za kibepari za Magharibi na zile za kikomunisti za Mashariki. Baada ya kueleza habari juu ya familia zake zote mbili, ambazo zilikuwa ni mitihani mitupu, Khamis anaelezea vipi aliweza kufika London, Uingereza, na kupata kazi za kutengeneza mashine za hisabu katika makampuni makubwa kadhaa ya mashine hizo.Akiwa huko London, ndiko Khamis alipojitambulisha na kuwa muumini wa siasa za mrengo wa kushoto baada ya kukutana na akina Abdulrahman Mohammed Babu na Ali Sultan Issa na kuhudhuria mikutano na makongamano yaliyokuwa yakiandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha Uingereza na huku akijishughulisha kuwasaidia baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Afrika Mashariki waliokimbilia London kuendelea na harakati zao za kuzikombowa nchi zao ili zipate uhuru. Khamis aliweza kuchambuwa kwa kina kabisa siasa ya Kibepari na siasa ya Kisoshalisti na kutambuwa kuwa siasa ya Kisoshalisti pekee ndiyo mkombozi wa nchi za Afrika kwa maendeleo yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Who reads Maisha yangu: Miaka minane ndani ya baraza la mapinduzi: Khaini au mhanga wa mapinduzi ??

It is typically read by self-directed learners exploring a subject in depth.

Common subject areas: history, science, philosophy, social sciences.

Author
Khamis Abdulla Ameir
Publisher
DL2A BULUU PUBLISHING
Published
2022
Language
SW
ISBN
9781092789097
Category
nonfiction
Subjects
History, African History, Humanities